Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mawaziri wakutana Kazakhstan kujadili maji

Mawaziri wakutana Kazakhstan kujadili maji

Mawaziri hii leo wanakutana mjini Astana Kazakhstan kwenye mkutano unaojadili masuala ya maji na matumizi ya nishati isoyochafua mazingira. Mkutano unaong’oa nanga hii leo na kumalizika mnamo tarehe 23 mwezi huu. Mkutano huo utawaleta pamoja wajumbe kutoka nchi 53 kutoka ulaya na pia Marekani, Canada na Israel.

Mkutano huo unazungumzia changamoto zilizopo katika kulinda maji na sehemu zingine pamoja na hatua zinazohitajika katika kuafikia matumizi na nishati safi. Mkutano huo umeandaliwa na tume ya uchumi ya Umoja wa Mataifa kwa Ulaya kwa ushirikiano na serikali ya Kazakhstan.