Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tanzania imepiga hatua kiasi kupunguza utapia mlo: Kikwete

Tanzania imepiga hatua kiasi kupunguza utapia mlo: Kikwete

Tanzania imepiga hatua kiasi katika kupunguza idadi ya watoto wenye utapia mlo amesema Rais wa nchi hiyo Jakaya Mrisho Kikwete.

Rais Kikwete ameuambia mkutano wa masuala ya chakula na lishe kwenye Umoja wa Mataifa jumanne kwamba kama ilivyo kwenye nchi nyingi zinazoendelea utapia mlo ni tatizo kubwa nchini Tanzania.

Amesema kwamba thelthi moja ya watoto walio na umri wa chini ya miaka mitano wanakufa na utapia mlo. Ameongeza kuwa katika kipindi cha miaka 35 iliyopita serikali imetekeleza mipango mbalimbali ya kuboresha lishe.

(SAUTI YA RAIS JAKAYA KIKWETE)

"Kutokana na hatua hizi hatua kiasi imepigwa, kwa mfano kati ya mwaka 1999 na 2010 idadi ya watoto kuduumaa imepunguzwa kutoka asilimia 44 hadi asilimia 35. Watoto wenye zito mdogo wamepungua kutoka asilimia 29 hadi 21 na wenye uupungfu wa damu imepungua ktoka aasilimia 72 hadi 59. Vilevile matatizo ya upungufu wa damu kwa wanawake wenye mri wa kuzaa yamepungua kutoka asilimi 50 hadi 40."