Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Bado wakimbizi zaidi wakwama nchini Libya

Bado wakimbizi zaidi wakwama nchini Libya

Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM linasema kuwa takriban wahamiaji 3000 kwa sasa wanatafuta makao kwenye kituo cha IOM wakati kunapoendelea kushuhudiwa mapigano kwenye mji wa Sebha chini Libya. Hata hivyo IOM ina wasi wasi kuhusu vile hali itakuwa kwenye kituo hicho kufuatia upungufu wa chakula unaoendelea kushuhudiwa .

Wahamiaji wengi wanatoka nchini Chad huku wengine wakitoka nchini Somalia, Eritrea, Nigeria, Misri, Jordan na Pakistan. Jumbe Omari Jumbe afisa wa IOM anafafanua.

(SAUTI YA JUMBE OMARI JUMBE)