Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Serikali ya Yemen yalaumiwa kwa kutumia nguvu dhidi ya waandamanaji

Serikali ya Yemen yalaumiwa kwa kutumia nguvu dhidi ya waandamanaji

Mamia ya watu wameuawa na maelfu ya wengine kujeruhiwa nchini Yemen baada ya serikali kutumia nguvu kupita kiasi ili kuzima maandamano nchini humo. Ripoti kutoka kwa ujumbe wa shirika linalohusika na masuala ya haki zabinadamu la Umoja wa Mataifa inasema kuwa maandamano ya amani ya kutoka kwa waandamanaji wanaotaka kukomeshwa kwa ufisadi na kuheshimiwa kwa haki za binadamu yamezimwa kwa kutumia nguvu.

Ujumbe huo unatoa wito wa kufanyika uchunguzi wa kimataifa ulio huru kuhusu madai hayo ya ukiukaji wa haki za binadamu. Hanny Megally kutoka ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa aliongoza ujumbe huo kwenda Yemen.

(SAUTI YA HANNY MEGALLY)