Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Shirika la kibinadamu nchini Yemen lashinda tuzo la Nansen la mwaka 2011

Shirika la kibinadamu nchini Yemen lashinda tuzo la Nansen la mwaka 2011

 

Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR hii leo limetangaza shirika linalohusika na masuala ya kibinadamu nchini Yemen kuwa mshindi wa tuzo la wakimbizi la Nansen Refugee Award. Tuzo hilo lenye thamani ya dola 100,000 linawatambua wafanyikazi 290 wa shirika hilo na mwanzilishi wake kutokana na kazi yao ya kuwasaidia maelfu ya wakimbizi na wahamiaji wanaowasili kando kando mwa pwani za Yemen kila mwaka baada ya kuvuka ghuba ya Aden kwa mashua. 

Wanapokimbia ghasia , Ukame na umaskini kwenye pembe ya Afrika maelfu ya wakimbizi na wahamijaji huweka maisha yao kwenye hatari mikononi mwa wasafirishaji haramu wa watu wakitumia mashua zilizochakaa. Flora Nducha na taarifa kamili. 

(RIPOTI YA FLORA NDUCHA)