Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ukame kulizorotesha eneo la Pembe ya Afrika

Ukame kulizorotesha eneo la Pembe ya Afrika

Pamoja na juhudi zinazochukuliwa na mashirika ya misaada ya kibanadamu yanayojaribu kukabiliana na hali ngumu inayojiri kwenye eneo la Pembe ya Afrika ambayo inaandamwa na ukame usiowahi kushuhudiwa, lakini hata hivyo hali inazidi kuzorota. Kwa mujibu wa maafisa wa shirika la utoaji misaada ya kibinadamu OCHA, eneo hilo linaandamwa na mkuanyiko wa matitizo kuanzia kuwepo kwa hali mbaya ya hewa, kuanguka kwa mavuno mpaka kuibuka kwa majanga mengine yanayotishia ustawi wa jamii.

Shirika la afya la Umoja wa Mataifa WHO limeonya juu ya uwezekano wa kusambaa kwa magonjwa ya mlipuko ambako hadi sasa watu 211 wamefariki dunia baada ya kuugua kipindupindu.

Mtaalamu mmoja Tarik Jasarevic amesema kuwa WHO sasa imeanza kutumia watalaamu pamoja na vituo vya afya vinavyotembezwa katika maeneo yanayokabiliwa na hali mbaya ikiwemo katika eneo la Kusini mwa Somalia.