Baraza la usalama, Katibu Mkuu Ban walaani mashambulio ya bomu Abuja

Baraza la usalama, Katibu Mkuu Ban walaani mashambulio ya bomu Abuja

Umoja wa Mataifa umelaani vikali mashambulizi yaliyolenga majengo ya umoja wa mataifa  nchini Nigeria ambako watu kadhaa walipoteza maisha na wengine kujeruhiwa. Bomu hilo lilitengwa kwenye gari lililipukia jengo la umoja wa mataifa lililoko kwenye mji mkuu Abuja ambako kunapatikana ofisi kadhaa za mashirika ya umoja wa mataifa.

Akizungumzia tukio hilo, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema kuwa kitendo hicho ni dhihaka dhidi ya watu waliojitolea kwa ajili ya kuwasaidia watu wengine.

Amesema amemtuma msaidizi wake Asha-Rose Migiro kuelekea nchini humo kwa ajili ya kuangalia athari zake.

(SAUTI YA BAN)