Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wahisani ni muhimu sana kwa mamilioni ya watu duniani:UM

Wahisani ni muhimu sana kwa mamilioni ya watu duniani:UM

Ijumaa ya tarehe 19 Agosti Umoja wa Mataifa na dunia kwa ujumla waliungana kuadhimisha siku ya kimataifa ya wahisani watu ambao mchango wao, kujitolea kwao na juhudi zao zimeokoa na zinaendelea kuokoa mamilioni ya watu katika maeneo yenye matatizo ya vita, njaa, majanga ya asili na kadhalika.

Kauli mbiu ya mwaka huu ni “watu kusaidia watu” na katika ujumbe maalumu wa siku hiyo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesisitiza kuwa katika wakati huu ambapo dunia inazongwa na matatizo, machafuko, na majanga wafanyakazi wa misaada ni muhimu sana na siku hii ni ya kuenzi mchango wao mkubwa.

(SAUTI YA BAN KI-MOON)

Mashirika ya Umoja wa Mataifa, ya kitaifa na kimataifa, NGO’s na hata watu binafsi wamekuwa wanaendelea kazi ya kujitolea na wengine hata kuweka maisha yao hatarini kwa ajili ya wengine kama alivyobaini mwandishi wetu nchini Burundi Ramadhani Kibuga.

(PKG RAMADHAN KIBUGA)