Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uwekezaji maji una manufaa kwa afya ya binadamu, usalama wa chakula na ukuaji wa uchumi:UNEP

Uwekezaji maji una manufaa kwa afya ya binadamu, usalama wa chakula na ukuaji wa uchumi:UNEP

Matokeo ya utafiti yaliyotolewa leo na Umoja wa Mataifa yanasema kuwekeza asilimia 0.16 ya pato la taifa kwenye sekta ya maji kutapunguza matatizo ya maji na kupunguza kwa nusu idadi ya watu wasio na fursa ya kupata maji safi ya kunywa na mahitaji muhimu ya usafi katika kipindi cha chini ya miaka minne.

Utafiti huo uliofanywa na shirika la Umoja wa Mataifa la mazingira UNEP unasema hivi sasa kushindwa kuwekeza katika huduma ya maji na kuyakusanya , kusafisha na kuyatumia tena ipasavyo kunachochea matatizo ya maji katika sehemu nyingi duniani na kuchangia hali ambayo mahitaji ya maji yatapindukia uwezo wa kuyapata katika miaka 20 ijayo.

Ripoti hiyo kuhusu uchumi unaojali mazingira imetolewa mjini Stockholm Sweeden ambako wiki ya kimataifa ya maji inafanyika na imesema kuwekeza katika usafi na maji ya kunywa kutimarisha mifumo ya usambazaji maji na kuwa na sema bora zitakazosaidia kupunguza gharama kubwa za kijamii na kiuchumi zitokanazo na upungufu wa maji.