Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watu milioni 12 wasio na utaifa wahitaji msaada wa haraka:UNHCR

Watu milioni 12 wasio na utaifa wahitaji msaada wa haraka:UNHCR

Watu milioni 12 duniani kote wanaishi bila uraia wa nchi yoyote hali inayowaweka katika mazingira ya kunyonywa na kunyimwa haki za msingi za binadamu limesema shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR. Ingawa kutokuwa na utaifa ni tatizo la dunia lakini linaathiri zaidi Kusini Mashariki mwa Asia, Asia ya Kati, Ulaya Mashariki na Mashariki ya Kati.

Kamishina mkuu wa UNHCR Antonio Guterres amesema watu wasio na uraia wanahitaji msaada kwani wengi wanaishi katika hali ya sintofahamu kisheria. Shirika hilo limesema bila utaifa watoto wa watu wasio na utaifa wanashindwa kupata elimu bora, huduma za afya na huduma zingine muhimu. Erika Feller kutoka UNHCR anasema kusambaratika kwa mataifa, kuwanyima watu uraia makusudi na ubaguzi wa kidini mara nyingi ni sababu kubwa za watu kutokuwa na utaifa.

(SAUTI YA ERIKA FELLER)

UNHCR inaziomba nchi zote duniani kutia saini mikataba takribani miwili ya Umoja wa Mataifa inayohusu kutokuwa na utaifa.