Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mashirika ya UM yanajiandaa kwa kimbuga Irene, Haiti

Mashirika ya UM yanajiandaa kwa kimbuga Irene, Haiti

Shirika la kimataifa la utabiri wa hali ya hewa WMO limesema kimbunga Irene kimeshika kasi na kupanda hadi daraja la 2 na maeneo kitovu ya kimbunga hicho ni Jamhuri ya Dominican na Haiti, na baadaye leo kinatarajiwa kupiga visiwa vya Turks na Caicos na Kusini mwashariki mwa Bahamas. WMO imesema tayari mipango imeandaliwa na inafuatilia kwa karibu kimbunga hicho Haiti na katikati mwa Bahamas. Clare Nullis ni afisa wa WMO

(SAUTI YA CLARE NULLIS)

Nalo shirika la kuratibu masuala ya kibinadamu OCHA limesema limeandaa misaada ya dharura ili kukabiliana na athari za kimbunga Irene. Limesema kuna uwezekano wa kuwepo mafuriko na maporomoko ya udongo hususani katika maeneo ya Kaskazini mwa Haiti. OCHA inasema inayo mahema 102,000, na imeandaa makazi ya muda 360 mjini Port-au-Prince ambako watu 50,000 wanaweza kuhifadhiwa kwa masaa 48.