Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Historia ya utumwa yaweza kusaidia watu kujifunza utu:UNESCO

Historia ya utumwa yaweza kusaidia watu kujifunza utu:UNESCO

Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la elimu sayansi na utamaduni UNESCO leo amewataka watu kujifunza historia ya udhalilishaji ya biashara ya utumwa ili kubaini utu wao na kuongeza juhudi za kupambana na unyanyasaji na ubaguzi wa rangi.

Bi Irina Bokova amesema kila mtu anapaswa kupewa uwezo wa kujifunza yaliyopita na kuyatafakari kama njia ya kuwa na msimamo wa pamoja. Bokova ameyasema hayo kwenye ujumbe maalumu kuadhimisha siku ya kimataifa ya kumbukumbu ya biashara ya utumwa na kukomeshwa kwake.

UNESCO imesema maadhimisho ya mwaka huu yana umuhimu mkubwa kwani ni mwaka wa 10 tangu kufanyika mkutano wa kimataifa dhidi ya ubaguzi wa rangi, kupinga ubaguzi huo, mauaji ya kuwalenga wageni na kutovumiliana. Mkutano huo ulifanyika mjini Durban Afrika ya Kusini ambako biashara ya utumwa ilitajwa kama ni uhalifu dhidi ya ubinadamu.