Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban alaani vikali shambulio la kujitoa muhanga msikitini Pakistan

Ban alaani vikali shambulio la kujitoa muhanga msikitini Pakistan

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amelaani vikali shambulio la kujitoa muhanga lililofanyika leo kwenye msikiti Kasjkazini Magharibi mwa Pakistan na kuuwa watu zaidi ya 40 na kujeruhi wengine zaidi ya 100. Duru za habari zinasema shambulio hilo limefanyika wakati wa swala ya Ijumaa kwenye msikiti wa kijiji cha Ghundi jimbo la Khybernchini Pakistan.

Katika taarifa yake Ban ametoa salamu za rambirambi kwa familia za waathirika na kuongeza kuwa amesikitishwa sana na shambulio hilo la makusudi kwenye nyumba ya ibada hasa katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhan, na zaidi ni kumtumia kijana mdogo kutekeleza uasi huo. Taarifa hiyo imesisitiza kwamba Umoja wa Mataifa utaendelea kushirikiana Pakistan katika juhudi zake za kupambana na ugaidi.