Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ofisi ya haki za binadamu yaonya juu ya kutoweka na kutekwa kwa watu Pakistan

Ofisi ya haki za binadamu yaonya juu ya kutoweka na kutekwa kwa watu Pakistan

Ofisi ya Kamishina Mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa imesema tangu mwaka 2007 imekuwa ikipokea ripoti za watu kutekwa, kutoweka, na mauaji nchini Pakistan.

Kwa mujibu wa ofisi hiyo wiki moja iliyopita kumekuwa na taarifa za kuawa kwa waandishi habari na wengine kutekwa Balochista na Kaskazini mwa Waziristan. Takwimu zinaonyesha kwamba 2010 waandishi 16 walitekwa na 9 kati yao kuawa, na hakuna uchunguzi wowote uliofanyika. Kamishina Mkuu amezitaka pande zote kusitisha mara moja ukiukaji huo wa haki za binadamu na kuchunguza visa hivyo kama anavyofafanua msemaji wa ofisi ya haki za binadamu Rupert Colville.

(SAUTI YA RUPERT COLVILLE)