Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mjadala kufanyika kuokoa maisha ya viumbe vilivyo hatarini :UM

Mjadala kufanyika kuokoa maisha ya viumbe vilivyo hatarini :UM

Kuokoa pembe za ndovu na vifaru kutoka kwa maharamia na wafanya biashara haramu ni miongoni mwa mada zitakazojadiliwa kwenye mkutano ulioandaliwa na mkataba wa Umoja wa Mataifa wa kulinda viumbe vilivyo katika hatari ya kutoweka CITES. Nchi 175 duniani zimetia saini mkataba huo. CITES hukutana kila baada ya miaka mitatu kujadili mapendekezo ya biashara ya nchi wanachama. John Scanlon ni katibu mkuu wa CITES anasema kudhibiti biashara kunaweza kusaidia viumbe vilivyo katika hatari ya kutoweka.

(SAUTI YA JOHN SCANLON)

Mkutano huo ambao utafanyika Geneva Switzerland unaongozwa na Rais Mwai Kibaki wa Kenya. Kenya ni muungaji mkono mkubwa wa mkataba huo kwani utalii unabeba sehemu kubwa ya uchumi wa nchi hiyo.