Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Balozi wa Uingereza kwenye UM apuuza mlinganisho wa ghasia za Uingereza na Syria

Balozi wa Uingereza kwenye UM apuuza mlinganisho wa ghasia za Uingereza na Syria

Balozi wa Uingereza ameitaka serikali ya Syria kusitisha matumizi ya nguvu na kuwakamata waandamanaji wanaouunga mkono demokrasia. Balozi Philip Parham ameyasema hayo mbele ya waandishi wa habari baada ya majadiliano kuhusu Syria kwenye baraza la salama mjini NewYork.

Parham pia amesisitiza haja ya uongozi wa Syria kusikiliza wito wa baraza la usalama na kanda nzima ya Mashariki ya Kati. Wakati huohuo amesema kuwa ni upuuzi kulinganisha ghasia za Uingereza na machafuko ya Syria, mlinganisho uliotolewa na balozi wa Syria kwenye Umoja wa Mataifa.

(SAUTI YA PARHAM)