Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wanawake Wasomalia wanaotafuta hifadhi wanakabliwa na ubakaji:UM

Wanawake Wasomalia wanaotafuta hifadhi wanakabliwa na ubakaji:UM

Mwakilishi maalumu wa Katibu Mkuu kuhusu masuala ya ukatili wa kimapenzi Margot Wallstrom amesema wakati hali ya njaa ikizidi kuwa mbaya nchini Somalia anatiwa hofu na ripoti za visa vya ubakaji kufuatia kukimbia kwa wimbi kubwa la Wasomali na kuuingia Kenya.

Vita, uukame na kukimbia makazi yao kunabainisha hali mbaya ya katili wa kimapenzi unaowakabili wanawake na wasichana. Amesema wakati wa safari ndefu kutoka Somalia kwenda kwenye kambi za wakimbizi nchini Kenya , wanawake na wasichana wanakabiliwa na mashambulizi, ikiwemo kubakwa vitendo vinavyotekelezwa na wanamgambo wenye silaha pamoja na wanyang’anyi, na wanapowasili kwenye kambi ya Dadaab matumaini yao ya usalama yanaghubikwa na hatari nyingine, ikiwemo ugumu wa maisha na hatari ya kubakwa.

Hata hivyo Bi Wallstrom amepongeza juhudi za serikali ya Kenya kwa kukabiliana na wimbi kubwa la wakimbizi wa Kisomali wanaoendelea kuingia nchini humo kwa maelfu, na ameitolea wito jumuiya ya kimataifa kuhakikisha msaada na fedha zinazotolewa kwa serikali ya Kenya na mashirika ya Umoja wa Mataifa kama UNHCR ili kukabiliana na hali hiyo.