Mamilioni ya watu waathirika kutokana na ghasia dhidi ya vituo na wahudumu wa afya
Mashambulizi dhidi ya mawafanyakazi wa afya, vituo na magari ya wagonjwa kwenye maeneo ya vita na machafuko yamewaacha mamilioni ya watu duniani bila huduma muhimu wanayoihitaji. Takwimu hizi ni kwa mujibu wa ripoti ya utafiti iliyotolewa leo katika mkutano na waandishi wa habari mjini Geneva na kamati ya kimataifa ya chama cha msalaba mwekundu ICRC.
Kwa mujibu wa utafiti huo uliofanywa kwenye nchi 16 duniani maisha ya mamilioni ya watu yanaweza kuokolewa endapo ufikishaji wa huduma za afya kuwa utaheshimiwa zaidi. Utafiti huo pia umebaini cha kusikitisha zaidi idadi kubwa ya watu wanakufa sio kwa mabomu ya barabarani au kupigwa risasi ni kwa sababu magari ya wagonjwa hayawezi kuwafikia kwa wakati muafaka. Hicham Hassan msemaji wa ICRC anasema jamii ya huduma za afya pekee haiwezi kukabiliana na changamoto hii ni jukumu la wadau wote.
(SAUTI YA HICHAM HASSAN)