Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban amtaka rais wa Syria kukomesha mabavu dhidi ya waandamaji

Ban amtaka rais wa Syria kukomesha mabavu dhidi ya waandamaji

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amemtaka rais wa Syria kukomesha vitendo vya dhuluma dhidi ya waandamanaji wanaopinga utawala wake akisema kuwa mamlaka hiyo inapaswa kuachana na vitendo hivyo mara moja.

Katika mazungumzo yake kwa njia ya simu na rais Bashar al-Assad Ban amemwambia rais huyo kuwa anapaswa kuchukua jukumu la kukomesha matumizi ya nguvu dhidi ya raia. Aidha ameelezea masikitiko yake hasa wakati huu ambapo kumekuwa na ongezeko kubwa la kuwashambulia waandamanaji ambao humiminika bara barani wakiukosoa utawala wa kiongozi huyo. Zaidi ya watu 2,000 wanaarifiwa kufariki dunia katika kipindi cha siku chache zilizopita.