Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM wachunguza madai ya mashumbulizi kwenye mitandao

UM wachunguza madai ya mashumbulizi kwenye mitandao

Uchunguzi umeanzishwa kufuatia madai kuwa mitandao ya Umoja wa Mataifa imekuwa ikiingiliwa. Wataalam wa masuala ya usalama wamedhibitisha kuwa kushambuliwa kwa mitandao kwa muda wa miaka mitano iliyopita kumeathiri mashirika mengi likiwemo shirika la Umoja wa Mataifa.

Msemaji wa Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Martin Nesirky anasema kuwa ofisi ya Umoja wa Mataifa mjini Geneva inajaribu kubaini iwapo mitandao hiyo iliingiliwa au la.

(SAUTI YA MARTIN NESIRKY)