Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hali ya njaa yaweza kusambaa:yaonya Umoja wa Mataifa

Hali ya njaa yaweza kusambaa:yaonya Umoja wa Mataifa

Mratibu wa masuala ya kibinadamu kwenye moja wa Matifa Valeria Amos hii leo anatarajiwa kuwahutubia waandishi wa habari hapa kwenye kikao kikuu cha Umoja wa Mataifa kuhusu hali katika pembe ya Africa. Umoja wa Mataifa unaonya kuwa njaa kwenye maeneo mawili nchini Somalia itasambaa katika eneo lote la kusini kwa muda wa mwezi mmoja au miwili ijayo ikiwa misaada haitaongezwa kwenye maeneo hayo.

Umoja wa Mataifa na washirika wake wanaungana kutoa misaada kwa watu milioni 12.4 kwenye pembe ya Afrika lakini hata hivyo mahitaji yanazindi kuongezeka huku idadi ya watu wanaohitaji misaada ikitarajiwa kuongezeka kwa asilimia 25.