Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Makundi ya kiislamu yakusanyika Tahrir Square

Makundi ya kiislamu yakusanyika Tahrir Square

Makundi ya kiislamu nchini Misri yalikusanyika katika eneo la Tahrir Square mwishoni mwa juma yakitaka kuwepo kwa taifa linaloongozwa na sheria za kiislamu za Sharia.Kulingana mkurugenzi wa kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa mjini Cairo Khawala Matter ni kuwa mkutano huo uliandaliwa na makundi yanayounga mkono demokrasia ili kuitisha mabadiliko ya haraka na kuandikwa kwa katiba kabla ya uchaguzi mwezi Oktoba.

Khawala Matter anasema kuwa wanaharaki hao walikuwa wamekubaliana kukutana kabla ya mwezi mtukufu wa Ramadhan.

(SAUTI YA KHAWALA MATTER)