Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

India yataka kusitishwa mapigano nchini Libya wakati wa mwezi wa Ramadhan

India yataka kusitishwa mapigano nchini Libya wakati wa mwezi wa Ramadhan

India imetoa wito wa kusitishwa mapigano nchini Libya wakati wa mwezi huu mtukufu wa Ramadhan inapochukua urais wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa. Kwa sasa mapigano yanaendeklea kwenye taifa hilo la kaskazini mwa Afrika wakati waasi wanapojaribu kumuondoa madarakani rais Muammar Gadhafi.

Mwezi Machi mwaka huu baraza la usalama la Umoja wa Mataifa lilipitisha azimio la kuruhusu Libya kushambuliwa kijeshi. Hardeep Singh Puri ni balozi wa India kwenye Umoja wa Mataifa.

(SAUTI YA HARDEEP SINGH PURI)