Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkuu wa IAEA atembelea kinu cha Fukushima nchini Japan

Mkuu wa IAEA atembelea kinu cha Fukushima nchini Japan

Mkuu wa shirika la kudhibiti nishati ya nuklia duniani Yukiya Amano ametembelea kinu cha nuklia cha Fukushima nchini Japan kufuatia kuharibiwa kwa kinu hicho tarehe 11 mwezi machi wakati kulipotokea tetemeko la ardhi pamoja na tsunami.

Amano amesema kuwa sababu kuu ya ziara yake ni kupata habari kamili kuhusu kinu hicho. Pia watu walioshuhudia ajali kwenye kinu hicho walimweleza amani kilichojiri na kile kinachofanywa na kampuni husika ili kurejesha hali ya kawaida. Akiwa nchini Japan Amano atakutana na waziri mkuu Naoto Kan na maafisa wengine wa ngazi za juu kujadili matokeo ya mkutano wa mwezi uliopita kuhusu usalama wa nguvu za nuklia.