Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Serikali zatakiwa kubuni ajira kwa vijana

Serikali zatakiwa kubuni ajira kwa vijana

Serikali kote duniani zimeshauriwa kuweka sera mwafaka ili kubuni nafasi za ajira kwa idadi ya vijana wanaotafuta ajira wanaozidi kuongezeka . Shirika la kazi duniani ILO linasema kuwa watu milioni 81 walio kati ya miaka 15 na 24 hawakuwa na ajira mwaka 2009.

Mkutano kuhusu ajira kwa vijana unaandaliwa mjini New York juma hili. Steven Kapsos kutoka ILO anasema hatua zinastahili kuchukuliwa mara moja.

( SAUTI YA STEVEN KAPSOS )