Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Idadi kubwa ya watu nchini Madagascar hawana chakula:De Schutter

Idadi kubwa ya watu nchini Madagascar hawana chakula:De Schutter

Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki ya kuwa na chakula Olivier De Shutter amesema kuwa mmoja kati ya watu wawili nchini Madagascar hana chakula. Akikamilisha ziara yake nchini humo De Schutter amesema kuwa vikwazo vilivyowekewa Madagascar vinachangia zaidi hali hiyo. Amesema kuwa kwa sasa Madagascar ina idadi kubwa zaidi ya watoto wanaosumbuliwa na utapiamlo duniani sawa na hali iliyopo nchini Afghanistan na Yemen.

Kufuatia mapinduzi yaliyotokea nchini Madagascar na kushindwa kwa mazunguzo ya upatanishi kulisababisha nchi hiyo kuwekewa vikwazo. De Shutterr ameongeza kuwa uamuzi wa Marekani wa kundoa Madagascar kutoka kwa makubaliono ya mandeleo ya bara ya Afrika kumesebabisha kupotea kwa ajira 50,000 kwenye sekta ya nguo ambayo ambayo ilikuwa nusu ya mauzo ya nje nchini Madagascar.