Ban aitaka Korea kuzisadia nchi maskini

Ban aitaka Korea kuzisadia nchi maskini

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ameishauri serikali na watu wa Korea kuwasaidia wasiojiweza duniani. Ban amesema kuwa Korea wakati mmoja ilisumbuliwa na njaa na umaskini , ilijitahidi kujiondoa kwenye mizozo na kujenga demokrasia. “kufuatia usaidizi kutoka kwa marafiki wema ikiwemo Marekani na Umoja wa Mataifa tulifaulu” amesema Ban .

Ameongeza kuwa leo hii Korea ina wajibu maalum wa kuzisaidia nchi maskini kutimiza ndoto zao za kimaendeleo , uongozi mwema na haki za binadamu pamoja na amani.