Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNHCR yaongeza misaada nchini Somalia

UNHCR yaongeza misaada nchini Somalia

Shirika la kuwahudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR limeongeza usambazaji wa misaada kwenye maeneo yaliyokumbwa na hali mbaya ya ukame kwenye pembe ya Afrika. UNHCR inasema kuwa hata kama kuwafikia wanaohitaji misaada linasalia kuwa changamoto kubwa , wakishirikiana na washirika wao katika maeneo hayo hadi sasa wamesambaza misaada kadha kwa karibu watu 90,000 mjini Mogadashu, Belet Hawa na Dobley Kusini magharibi mwa Somalia.

UNHCR pia inajaribu kufuatilia kuhama kwa watu na usalama kwenye njia wanazopitia wakielekea kambi ya Dolo Ado nchini Ethiopia na Daadab nchini Kenya. Adrian Edwards ni msemaji wa UNHCR.

Mkurugenzi mkuu wa shirika la mpango wa chakula duniani WFO Josette Sheran anaondoka hii leo kuelekea eneo hilo ambapo ziara yake itaanzia nchini Ethiopia, Kenya na kisha Somalia. Naye Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki  -moon ameelezea wasiwasi  wake kuhusu hali ilivyo kwenye pembe ya Afrika.