Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Iraq inapaswa kuboresha mikakati yake ili kuleta ustawi wa maisha kwa vijana-UM

Iraq inapaswa kuboresha mikakati yake ili kuleta ustawi wa maisha kwa vijana-UM

Mwanadiplomasia wa Umoja wa Mataifa anayehusika na Iraq, ameitolea mwito nchi hiyo kuendeleza mifumo na mikakati ili kujenga ulinzi imara katika maeneo ya uchumi na ustawi kwa vijana .

Akijadilia ripoti mpya ya maendeleo inayoangazia maisha ya vijana, Mjumbe huyo wa Umoja wa Mataifa amesema kuwa kuna haja ya kuleta mageuzi ya kimaendeleo hasa kwa kuzingatia kuwa takwimu nyingi zinaonyesha jinsi vijana hao walivyoachwa nyuma. Ad Melkert amesema kiwango cha ujinga, ukosefu wa ajira miongoni mwa vijana nchini humo bado kipo juu. Kulingana na ripoti hiyo vijana wenye umri kati ya miaka 15 hadi 29 ambao hawana ajira wanafikia zaidi ya asilimia 57.