Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM wawapelekea misaada wakimbizi kutoka Somali walio nchini Kenya

UM wawapelekea misaada wakimbizi kutoka Somali walio nchini Kenya

Misaada imeanza kuwasili kwenye mji mkuu wa Kenya Nairobi kama moja ya jitihada za shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR za kuwasaidia maelfu ya wakimbizi kutoka Somalia ambao wamechukua hifadhi kwenye kambi za wakimbizi nchini Kenya. Ndege ya kwanza iliyosheheni tani 100 za hema zitakazopelekwa kambi ya Daadab tayari ishatua Nairobi.

(SAUTI YA GEORGE NJOGOPA)