Kamishna mkuu wa UNHCR apongeza watu wa Sudan Kusini kwa kupata uhuru

9 Julai 2011

Kamishina mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR Antonio Guterres amesema wakati historia inapoandimkkwa na taifa la Sudan kusini, UNHCR inaungana na mashirika mengine ya kimataifa na watu kote duniani kulikaribisha taifa hilo jipya.

Amesema kuwa takriban watu 350,000 waliokuwa wakimbizi ambao wamerejea Sudan Kusini kwa miaka sita iliyopita na maelfu wa wenyeji wa Sudan Kusini ambao wanaoungana nao kitakuwa kitu muhimu kwa kukua kwa taifa hilo jipya .

Guterres ameongeza kuwa amefurahishwa na hatua ya bunge la Sudan Kusini ya kupitisha mswada unaozuia mtu kukosa uraia na kuongeza kuwa anaamini serikali ya Sudan Kusini itakuwa na sera za kuzuia watu waliosalia Kaskazini kukosa uraia.

 

♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter