Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Maatatizo ya kisaikolojia yawasumbua wahamiaji wanaokimbia Libya

Maatatizo ya kisaikolojia yawasumbua wahamiaji wanaokimbia Libya

Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM linasema kuwa wahamiaji wanaokimbia Libya na wanaousumbuliwa na matatizo ya kisaikolojia hawatapa nafuu inavyotakikana bila kuhudumiwa mara wanapowasili nyumbani au kwenye nchi zingine. Kati ya karibu watu milioni 1.2 ambao wamekimbia Libya tangu kuanza kwa mzozo mwezi Februari mwaka huu zaidi ya watu 600,000 kati yao ni wahamiaji ambao wengi wamepitia matatizo makubwa walipokuwa wakikimbia ghasia hizo.

Wengi wa wahamiaji hao wanaonekana wakiwa na hofu na wasiwasi mkubwa huku wanaohitaji huduma zaidi wakiwa ni wanawake na watoto. Pia wenyeji wa kusini mwa jangwa la Sahara wamesumbuliwa na vitendo vilivyokuwa vikiendeshwa Libya wakati wa mzozo huo vikiwalenga raia wa Chad kwa madai kuwa walikuwa mamluki.