Wafanyakazi wawili wa WFP waliotoweka wapatikana wakiwa salama

30 Juni 2011

 

 

 

Shirika la mpango wa chakula duniani WFP limedhibitisha kuwa wafanyikazi waliokuwa wametangazwa kutoweka wamepatikana wakiwa salama. Wafanyikazi hao walitoweka baada ya kutokea kisa kwenye eneo moja la kisomalia Mei 13 mwaka huu.

WFP imesema kuwa wafanyikazi hao wamesafirishwa hadi mjini Addis Ababa ambapo wanapokea huduma za matibabu na ushauri na kujumuishwa na familia zao. Wafanyikazi hao walipatikana kufuatia ushirikino kati ya WFP na Umoja wa Mataifa pamoja na tawala za kitaifa na kimaeneo.

 

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa UNGA76 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter