Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mtaalamu wa masuala ya ubaharia wa Japan achaguliwa kuongoza IMO

Mtaalamu wa masuala ya ubaharia wa Japan achaguliwa kuongoza IMO

Afisa mmoja kutoka Japan ambaye anataalamu ya kutosha juu ya masuala ya ubaharia anatazamiwa kuchukua wadhifa kwenye kitengo cha Umoja wa Mataifa kinachohusika na masuala ya usalama wa meli.

Koji Sekimizu mwenye umri wa miaka 59 ametangazwa kuwa ndiye atayekuwa mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa juu ya masuala ya baharini IMO kuanzia January 1 mwakani, akichukua pahala pa Efthimios E. Mitropoulos anayemaliza muda wake.Anatazamiwa kuchika wadhifa huo kwa muda wa miaka minne.Mkuu huyo mpya alichaguliwa katika kikao baraza la IMO kinachoendelea sasa. Hata hivyo atahitaji kudhibitishwa hapo mwezi Novemba.