Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Huenda mapigano katika eneo la Abyei na Kordofan kusini yakasambaa

Huenda mapigano katika eneo la Abyei na Kordofan kusini yakasambaa

Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa imesema kuwa hali iliyopo kwa sasa kwenye maeneo ya mpaka kati ya Sudan Kaskazini na Kusini huenda ikalitumbukiza taifa hilo kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Naibu kamishna mkuu wa tume ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa Kyung-wha Kang anasema kuwa mapigano yanayoendelea katika eno la Abyei na Kordofan Kusini huenda yakasambaa kwenda sehemu zingine na ni lazima yazitishwe. Bi Kang anasema kuwa hata kama watu wa Sudan Kusini wanasubiri kwa hamu uhuru wao kila hatua lazima ichukuliwa kuzuia ghasia za kijamii ambazo zimesababisha vifo vya watu 1400 tangu mwanzo wa mwaka huu.

(SAUTI YA KYUNG WHA KANG)

Kanga amesema kuwa zaidi ya watu 70,000 wamekimbia makwao katika eneo la kusini mwa Darfur siku za hivi majuzi na kwa sasa wanahitaji usaidizi wa dharura.