Skip to main content

Ban akaribisha makubaliano kati ya (SPLM-NORTH) na serikali ya Sudan

Ban akaribisha makubaliano kati ya (SPLM-NORTH) na serikali ya Sudan

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataiafa Ban Ki moon amekaribisha kutiwa sahihi kwa makubaliano kati ya serikali ya Sudan na kundi la kaskazini la Sudan People’s Liberation Movement (SPLM-NORTH ) ya kuwa na ushirikiano wa kisiasa kati ya chama cha Nation Congress Party (NCP) na pia kuhusu mipango ya kisiasa na amani kwenye majimbo ya Blue Nile na Kordofan Kusini.

Ban amepongeza pande zote kwa kufikia makubaliano hayo ambapo pia amazishauri pande hizo kumaliza ukatili unaoendelea kwenye jimbo la Kordofan Kusini bila kuchelewa. Ban pia ameishukuru kamati ya muungano wa Afrika iliyokuwa chini ya uongozi wa rais wa zamani wa Afrika Kusisini Thabo Mbeki na washirika wengine kwa kusaidia kuafikiwa kwa makubaliano hayo.