Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ukiukwaji wa haki za binadamu umefanyika Ivory Coast:UM

Ukiukwaji wa haki za binadamu umefanyika Ivory Coast:UM

Ukiukwaji wa haki za binadamu bado unafanyika nchini Ivory Coast licha ya kumalizika kwa mtafaruku wa kisiasa na ghasia zilizochochewa na matokeo ya uchaguzi wa Rais yaliyozua utata Desemba 2010.

Hii ni sehemu ya hitimisho lililofikiwa na tume ya kimataifa ya uchunguzi kuhusu Ivory Coast katika ripoti yake iliyowasilishwa kwenye baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa mjini Geneva hii leo. Tume hiyo imesema kwamba tangu mwezi Machi mwaka huu wafuasi na wanamgambo wanaomuunga mkono Allasane Ouattara wamekuwa wakitekeleza vitendo vya ukiukaji wa haki dhidi ya wale wanobainika kuwa ni wa upande wa upinzani. Mwenyekiti wa tume hiyo ni Vitit Muntarbhorn ambaye anasema vitendo vibaya kabisa vya ukiukwaji wa haki vimekuwa vikifanyika kwenye mji wa biashara wa Abdijan kwenye taifa hilo la Afrika ya Magharibi.

(SAUTI YA VITIT MUNTARBHORN)