Skip to main content

Bado watoto wanazidi kuingizwa kwenye ajira mbaya:ILO

Bado watoto wanazidi kuingizwa kwenye ajira mbaya:ILO

Shirika la kazi duniani ILO linasema kuwa zaidi ya watoto milioni 115 kote duniani wanafanya kazi zisizofaa. Kwenye ripoti iliyotolewa wakati wa kuadhimishwa siku ya kimataifa ya kupinga ajira ya watoto ILO inasema kuwa utafiti kutoka nchi zinazoendelea na zilizostawi unaonyesha kuwa kila siku na kila dakika mfayikazi mototo huwa anajeruhiwa au kuugua ugonjwa unaohusina na kazi anayofanya. 

Ripoti hiyo inasema kuwa zaidi ya asilimia sitini ya watoto wanaofanya kazi kama hizo ni wa kiume na mara nyingi ajira hiyo huwa inahusiana na sekta ya kilimo. Sasa ILO inaelezea wasi wasi wake kuwa hali mbaya ya uchumi iliyopo duniani hueda ikatatiza juhudi za kuangamiza ajira mbaya za watoto ifikapo mwaka 2016.