Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la haki za binadamu lajadili uzuiaji wa haki za binadamu

Baraza la haki za binadamu lajadili uzuiaji wa haki za binadamu

Baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa hii leo limefanya mjadala kuhusu haki za wanawake huku kamati iliyoteuliwa ikijadili mwanya uliosalia katika kuangamiza dhuluma dhidi ya wanawake. 

Akiijulisha kamati hiyo mkuu wa tume ya haki za binadamu ya Umoja Navi Pillay amesema kamati hiyo ina jukumu  la kuzuia dhuluma dhidi ya wanawake ikiwa ndilo suala kuu katika kupambana na dhuluma dhidi ya wanawake ambapa amesema kuwa kuzuia dhuluma dhidi ya wanawake ni suala linalostahili kuingiliwa kati kisiasa na kiuchumi.