Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mapigano makali yaripoti kwenye jimbo la Kordofan kusini nchini Sudan

Mapigano makali yaripoti kwenye jimbo la Kordofan kusini nchini Sudan

Mapigano makali kati ya vikosi vya wanajeshi wa Sudan na vile vya Sudan People’s Liberation Army (SPLA) yameripotiwa kwenye jimbo la Kordofan kusini na kusambaa hadi mji mkuu wa jimbo hilo Kadugli ikiwemo miji mingine midogo na vijiji. 

Takriban kati ya watu 3000 na 40,000 wanaaminika kuukimbia mji wa Kadugli huku kati ya watu 6000 na 10000 wakipiga kambi kando mwa barabara kati ya makao ya ujumbe wa umoja wa mataifa nchini Sudan na uwanja wa ndege. 

Hospitali ya Kadugli kwa sasa haitoi huduma yoyoTe huku wale waliopiga kambi kando ya barabra wakiwa ndio wanapata huduma za matibabu. Shirika la afya duniani WHO linampango ya kutuma bidhaa za matibau zitakazotoa huduma kwa watu 30,000 kwa muda wa miezi mitatu.