Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Waliokimbia mapigano mjini Abyei wahitaji msaada ya dharura

Waliokimbia mapigano mjini Abyei wahitaji msaada ya dharura

Watu zaidi wanaokimbia mji wa Abyei wanaendelea kuandikishwa huku kukiripotiwa uhaba wa mafuta na usalama masuala yanayotatiza utoaji wa misaada kwenye maeneo inayohitajika zaidi.

Wafanyikazi wa shirika la kimataifa la uhamiaji IOM na washirika wengine wanaendelea na usambazaji wa misada ya kuokoa maisha lakini wanasema kuwa wanakabiliwa na changamoto nyingi kutokana na ukosefu wa mafuta na kuendelea kwa mzozo. Wafanyikazi wa IOM wanasema kuwa asilimia 56 ya waliolazimika kuhama makwao ni wanawake na asilimia 21 ya watoto walio chini ya umri wa miaka minne. Wote hao wanahitaji makao , chakula na usaidizi mwingine.

Jumbe Omari Jumbe ni msemaji wa IOM