Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Zaidi ya watu bilioni moja wenye ulemavu wanakabiliwa na vikwazo kila siku

Zaidi ya watu bilioni moja wenye ulemavu wanakabiliwa na vikwazo kila siku

Shirika la afya duniani WHO na Bank ya dunia leo wametoa makadirio mapya ya kimataifa yasemayo zaidi ya watu bilioni moja wana aina fulani ya ulemavu . Mashirika hayo yamezitaka serikali kufanya juhudi za kuwezesha mifumo ya huduma na kuwekeza katika mipango maalumu ili kuwawezesha na kuwasaidia watu wenye ulemavu.

Ripoti hiyo ya kwanza kabisa ya kimataifa kuhusu watu wenye ulemavu inatoa makadirio ya kwanza ya watu wenye ulemavu kwa miaka 40 na inatoa mtazamo wa hali ya ulemavu duniani.

Utafiti mpya unaonyesha kwamba moja ya tano ya makadirio ya kimataifa ya watu wanaoishi na ulemavu ambao ni kati ya watu milioni 110 hadi milioni 190 wanakabiliwa na changamoto kubwa kila siku katika maisha yao. Ripoti inasema nchi chache tuu ndio zenye mipango tayari ya kukabiliana na mahitaji ya watu wenye ulemavu.

Kwa mujibu wa mkurugenzi mkuu wa WHO Margaret Chan vikwazo wanavyokabiliana navyo ni pamoja na unyanyapaa na ubaguzi, ukosefu wa huduma za afya, huduma za usafiri, uwezo wa kuingia katika baadhi ya majengo, na teknolojia ya mawasiliano na matokeo yake wanakuwa na afua duni, elimu ndogo, hawana mafanikio na fursa chache za kiuchumi, na umasikini mkubwa kuliko wengine.

(SAUTI YA DR……)