Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watoto wengi wametawanywa na bomoabomoa ukingo wa magharibi

Watoto wengi wametawanywa na bomoabomoa ukingo wa magharibi

Shirika la Umoja wa Mataifa la msaada kwa wakimbizi wa Kipalestina UNRWA limetoa takwimu zake za mwezi zinazohusiana na vitendo vya bomoabomoa na kuhamisha watu kwa nguvu vinavyofanywa na Israel kwenye Ukingo wa Magharibi. Takwimu hizo zinaonyesha kwamba watoto wengi wametawanywa na bomoabomoa hiyo.

Chris Gunness ambaye ni msemaji wa UNRWA amesema bomoabomoa hiyo imeshuhudia watoto 67 wakitawanywa mwezi May, ambapo 64 katika eneo la Area C na wengine watatu Jerusalem Mashariki. George Njogopa anaripoti.

(RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)