Matumizi ya tumbaku yaongezekakatika nchi zinazoendelea

31 Mei 2011

Shirika la afya duniani WHO linasema wakati matumizi ya bidhaa za tumbaku yakianza kupungua katika mataifa yaliyoendelea nchi zinazoendelea ambazo nyingi ni masikini matumizi yanaongezeka.

Shirika hilo limeonya kwamba watu takribani milioni 6 wanakufa kila mwaka duniani kwa sababu ya maradhi yatokanayo na athari za tumbaku ikiwemo saratani na magonjwa ya moyo, limesema endapo hatua madhubuti hazitochukuliwa basi idadi ya vifo na maradhi hayo yasiyo ya kuambukiza itaongezeka. Katika nchi zinazoendelea serikali zinajitahidi kudhibiti lakini sio kwa kasi inayostahili.

Vijana hawa toka kenya wana maoni mbalimbali kuhusu matumizi ya bidhaa za tumbaku ikiwemo sigara.

(MAONI KENYA)

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud