Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kufikia malengo ya milenia ya afya bado ni mtihani mkubwa kwa nchi kama Burundi

Kufikia malengo ya milenia ya afya bado ni mtihani mkubwa kwa nchi kama Burundi

Ulimwengu umeadhimisha aprili 7 siku ya afya duniani, ikiwa imesalia miaka nne tuu kabla ya muda wa kutimiza malengo ya mileani hapo 2015.

Burundi kama zilivyo nchi nyingi za Afrika inasema juhudi zinafanyika ili kustaawisha afya ya wananchi, lakini changamoto bado ni nyingi kuweza kufikia malengo ya maendeleo ya milenia hasa ya afya kutokana na kuibuka maradhi mengi ,uhaba wa vifaa , upungufu wa madawa na umasikini uliokithiri kwa wananchi kuweza kuumudu gharama za matibabu.

Kwa mujibu wa shirika la afya duniani WHO, kauli mbiu mwaka huu Burundi na duniani kote ni " kuhakikisha hatua zinachukuliwa haraka kudhibiti usugu wa dawa ,vita vikielekezwa katika kupambana na dawa za magendo, tabia sugu ya wananchi kujitibu wenyewe pasina kuonana na madaktari na matumizi ya kupindukia ya dawa.

Kutoka Bujumbura,Muandishi wetu Ramadhani KIBUGA ametuandalia makala hii ,ungana naye.

(MAKALA NA RAMADHAN KIBUGA)