Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watu wa asili wana haki ya kupata maji:UM

Watu wa asili wana haki ya kupata maji:UM

Kongamano linalohusisha watu wa asili ambalo linaratibiwa na umoja wa mataifa limetoa kilio chake kuhusiana adha wanayokumbana nayo watu hao wa asili hasa kwenye ufikiaji miradi ya kimaendeleo.

Wajumbe kwenye kongamano hilo wamedai kuwa watu wa asili wameendelea kubaguliwa kwa kutoshirikishwa kikamilifu kwenye miradi mingi ya kimaendeleo licha kwamba maeneo mengi inayozunguka jamii hiyo kubarikiwa na utajiri mkubwa wa malighafi.

Wametolea mfano vitu kama rasilimali muhimu ambazo zinashabiana na utamaduni wao kupatikana kwa wingi kwenye maeneo yao, lakini chakushangaza ni kuwa kundi hilo la watu bado limeendelea kupuuzwa.

Wamesema rasilimali kama maji ambayo ni chanzo kikubwa cha uendelezaji wa miradi ya kimaendeleo kupatikana, lakini hata hivyo hakuna mamlaka iliyotilia uzito wowote