IOM kusafirisha mamia ya wahamiaji waliokwama jangwani Chad

IOM kusafirisha mamia ya wahamiaji waliokwama jangwani Chad

Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM kuanzia mwishoni mwa wiki hii wataanza kuwasafirisha maelfu ya wahamiaji waliokwama jangwani mpakani mwa Chad na Niger.

Wahamiaji hao ni wale wanaokimbia machafuko Libya, na kujikuta wamekwama kwa kukosa urafiri wa kuwafikisha Chad. Kwa mujibu wa IOM wahamiaji hao wengi kutoka Afrika Kusini mwa jangwa la Sahara watasafirishwa kwa njia ya malori na watakuwa na safari ngumu na ndefu ya zaidi ya siku 20 jangwani.

Afisa habari na mawasiliano wa IOM Jumbe Omari Jumbe amemfahamishamtangazaji wa Idhaa hii Alice Kariuki kuhusu adha hiyo kwa wahamiaji.