Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watu wa asili wanaoishi msituni wa congo wanakabiliwa na kifo wasipolindwa:UM

Watu wa asili wanaoishi msituni wa congo wanakabiliwa na kifo wasipolindwa:UM

Jamii ya watu wa asili wanaoishi msituni nchiniJamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wanakabiliwa na kifo endapo sheria zilizowekwa kuwalinda wao na maisha yao zisipotekelezwa.

Onyo hilo limetolewa na afisa wa Umoja wa Mataifa anayefanya kazi nchini humo kwenye kongamano la kimataifa la watu wa asili linaloendelea kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa hapa New York.

Bwana David Lawson ambaye ni mwakilishi wa shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu duniani UNFPA nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo amesema uelimishaji kwa niaba ya jamii za watu wa asili umesaidia kupitishwa sheria za kulinda jamii hiyo mwezi februari mwaka huu. George Njogopa anaripoti.

(RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)