Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM umezindua kampeni kwenye Facebook ya kuchagiza muingiliano wa tamaduni

UM umezindua kampeni kwenye Facebook ya kuchagiza muingiliano wa tamaduni

Katika kuadhimisha siku ya kimataifa ya muingiliano wa tamaduni , shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na utamaduni UNESCO kwa ushirikino na shirika la Umoja wa Mataifa la muungano wa ustaarabu UNAOC wanazindua kampeni ya kimataifa kuunda vuguvugu kuanzia ngazi cha chini katika jamii kuchagiza maingiliano ya tamaduni.

Kampeni hiyo inatoa wito kwa watu binafsi kuchukua hatua ya kufanya kitu kimoja ambacho ni muhimu katika maisha yao kuchagiza muingiliano wa tamaduni kwa kujifunza kuhusu tamaduni nyingine kwa kupitia filamu, chakula, au makumbusho, kujifunza kuhusu nchi zingine au kutumia muda wao fulani kujitolea kwa kampeni hiyo. Alice Kariuki anaripoti

(RIPOTI YA ALICE KARIUKI)