Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kongomano la kimataifa la afya kutathmini magonjwa yasiyo ya kuambukiza

Kongomano la kimataifa la afya kutathmini magonjwa yasiyo ya kuambukiza

Kongamano la kimataifa la afya linaendelea mjini Geneva na leo linatupia macho suala la magonjwa yasiyo ya kuambukiza. Washiriki wa kongamano hilo kutoka kila pembe ya dunia nchi wanachama wa shirika la afya duniani WHO watapewa taarifa ya hali ya sasa ya maradhi hayo, hatua zilizopigwa na matokeo ya mikutano na matukio ya kikanda ya kudhibiti magonjwa hayo ikiwa ni pamoja na mkutano wa kimataifa wa mawaziri wa afya.

Mkutano huo pia utatoa fursa kwa nchi wanachama kujadili maandalizi ya mkutano wa ngazi ya juu wa baraza la Umoja wa Mataifa kuhusu masuala ya afya.

Maradhi hayo yasiyo ya kuambaukiza ambayo ni pamoja na kisukari, kiharusi, shinikizo la damu na saratani yanakatili maisha ya mamilioni ya watu kila mwaka, na pia yanaongeza mzigo mkubwa wa gharama za matibabu hususani kwa nchi masikini.